Wizara ya fedha imeweka mikakati itakayohakikisha, pesa zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika bajeti, na zile za miradi ya kukwamua uchumi wa nchi kutokana na athari za mporomoko wa kiuchumi duniani, zitatumika vizuri na kwa muda uliokusudiwa. Aiyakariri haya, waziri wa fedha Uhuru Kenyatta alisikitika kuwa kiasi kikubwa cha pesa zilizotolewa katika bajeti ya ziada mwaka huu, zitarejeshwa kwa wizara ya fedha kwa makadirio ya bajeti ya mwaka ujao kwa kuwa pesa zenyewe hazijatumika kikamilifu.