Msongamano mkubwa wa magari umeshuhudiwa kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi kufuatia kufungwa kwa sehemu ya barabara hiyo katika daraja la Mto Mawe eneo la Athi River kufuatia ukarabati unaoendelezwa.
Kwa mujibu wa OCPD wa Machakos Joseph Tenai, wahandisi wa kampuni ya kukarabati barabara ya Uchina wanaendelea kukarabati sehemu ya daraja hilo, na kuwashauri wamiliki wa magari madogo kutumia barabara ya Kangundo-Machakos.
Magari makubwa aina ya trela yametakiwa kuegeshwa kando ya barabara ili kuwapa nafasi wahandisi wakamilishe shughuli hiyo.