Mswada wa kufanikisha  kubuniwa kwa sheria ya kusimamia kura ya maamuzi umewasilishwa katika bunge.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati, mswada huo unalenga kujaza mapengo yaliyopo kisheria  katika kuandaa na kusimamia kura ya maamuzi iwapo itahitajika.

Kwa muda sasa kumeendelea michakato mbalimbali ya kushinikiza kura ya maamuzi, wa muhimu zaidi ukiwa ule unaoendelezwa na jopo la mapatano ambalo linakusanya maoni kuhusu njia bora zaidi ya kushughulikia changamoto za utangamano nchini.

Familia moja kutoka Nyahera Kaunti ya Kisumu inamtafuta kijana aliyepotea mwezi uliopita akiwa shule moja kwenye Kaunti ya Vihiga.

Joseph Olang' mwenye umri wa miaka 12 alipotea mwezi uliopita siku mbili baada ya kujiunga na shule hiyo ya walemavu ya Chamakanga Vihiga. John Gordon Olilo ni babuye.