Mamlaka ya Kitaifa ya Uhifadhi wa Mazingira NEMA Jumanne tarehe 24 mwezi Aprili inatarajiwa kutekeleza agizo la kufungwa kwa kichinji cha Kiamaiko jijini Nairobi. NEMA imesema sababu ya kuchukua hatua hiyo ni uchafuzi wa Mto Nairobi kufuatia uchafu unaotoka kwenye kichinjio hicho. Serikali ya Kitaifa na ya kaunti imejitolea kuusafisha mto huo

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa NEMA Evans Nyabuto, kichinjio hicho kitafungwa hadi kitakapozungatia kanuni zilizowekwa kuhusu utupaji taka. Shughuli ya kuusafisha Mto Nairobi ni mojawapo ya mikakati ya serikali hizo mbili kuboresha sura ya jiji la Nairobi.