Kampuni ya Procter &Gamble inayotengeneza vitambaa vya hedhi aina ya Always, imeanza shughuli kuwasabbazia wasichana elfu 10,896 vitambaa hivyo katika maeneo mbalimbali nchini.
Chini ya mpango kwa jina “Always Keeping Girls in Schools” wasichana hao watapewa vitambaa vitakavyodumu kwa mwaka mmoja. Vilevile watapewa nguo za ndani na mafunzo kuhusu kubalekhe na ujuzi wa masuala mbalimbali ya maisha.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mary Ndungu, mpango huo unawashirikisha wazazi katika majadiliano kuhusu tamaduni mbalimbali kama vile ndoa na mimba za mapema, masuala ambayo huathiri masomo pamoja na afya ya watoto wao wa kike.