Kusema kweli, ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Pharaoh. Kanisa ya Kikatoliki imekumbwa na madai ya unyanyasaji wa watoto kwa muda mrefu sana. Azimio ya Papa Francis kuiunda idara itakayowajibika kuchunguza maaskofu wasiowachukulia hatua kwa waliochini yao wanaonyanyasa watoto ni jambo bora kwa ujumla. Matokeo ya idhini hii, yatajulikana baadaye.

Hoja kuu ni kama kutakuwa na uwazi katika uchunguzi utakaofanywa na idara hii. Changamoto kuu ni kama kanisa ya kikatoliki inaweza kujichunguza yenyewe huku wanaoshukiwa kufanya maovu kwa watoto wakiwa wasimamizi na vigogo kwenye kanisa hiyo.

Jambo la pili ni kama idara hii itawajibika kupiga ripoti kwa polisi na idara za kisheria wanapopata fununu ya unyanyasaji wa watoto. Miaka ya nyuma, kanisa ya kikatoloki imefumba macho huku kukiwa na unyanyasaji wa wazi ukiendelea. La tatu ni kujuwa kama uchunguzi kwa wanyanyasaji utapanuliwa kujumuisha wanyanyasaji wote na sio wale wa watoto pekee.

Papa Francis amejaribu kufanya mabadiliko kadha lakini itabidi athibitishe kwa uwazi uchunguzi unaofanywa kwa washukiwa. Pia ionekane bayana kuwa hatua kali za kisheria zinachukuliwa kwa wanaopatikana na hatia.

Professor David O. Monda

Dept. of Social Science

National University - California.