Jopo litakalowachunguza na kuwateuwa makamishna wa tume ya uchaguzi na mipaka limeapishwa hii leo na jaji mkuu Willy Mutunga.waziri wa sheria mutula kilonzo alieleza jopo hilo kuwa darubini ya wakenya inawalenga katika kuhakikisha kuwa wameteuwa makamishna watakaorejesha imani ya wakenya kuhusiana na tume ya uchaguzi nchini.pia aliwaomba kujitenga na shinikizo za kisiasa, ukabila na kubuni tume isiyoegemea upande mmoja. Jopo hilo lina siku saba kutangaza nafasi hizo.