Kibaki on 2012 politics - Swahili
By Standard Digital
| Aug. 2, 2011
Rais mwai Kibaki amesema kuwa hatashurutishwa na yeyote kumtaja mrithi wake. Semi hizi zimepokelewa kama pigo kwa baadhi ya wanasiasa hasa wakati huu ambapo kampeini zimeonekana kushika kasi huku kila mmoja akikisia kuwa fulani wa fulani huenda akatajwa kama mrathi wa Kibaki pindi atakapoondoka mamlakani. Kufuatia hilo rais amewataka wanasiasa kukoma kueneza kampeni wakati huu na badala yake kuangazia masuala yanayomfaidi mwananchi.