Uongozi mbaya ndio chanzo kikuu cha ukosefu wa amani barani Afrika na kimataifa. Haya ni kwa mujibuwa kongamano la kimataifa kuhusu amani la mwaka wa 2010 lililoandaliwa  jijini

Nairobi na ambalo liliwaleta pamoja viongozi kutoka sehemu mbalimbali duniani. Viongozi wote waliohutubu walisisitizia hoja ya kuangamiza umaskini na kuboresha ustawi Hususan katika bara hili la Afrika lakini kuafikiana kuwa yote haya hayawezekani pasi na kuwepo amani. Mwanahabari wetu Carol Nderi alihudhuria kongamano

hilo na kutuandalia taarifa ifuatayo.