Katika kile kilisubiriwa kwa hamu kuona iwapo watamkinga mwenzao, idara ya mahakama leo ilionyesha kuwa kweli hii ni kenya mpya. Baraza kuu la idara ya mahakama JSC limependekeza kuwa naibu jaji mkuu Nancy Barasa asimamishwe kazi, na rais kibaki aunde jopo kazi la kuchunguza mwenendo wake kutokana na lile tukio linalodaiwa alimtisha bawabu rebecca kerubo kwa bastola. Kiongozi wa mashtaka wa serikali keriako tobiko tayari alikuwa ameikosoa idara ya polisi, akisema iliendesha uchunguzi wake kiholela, na ndio maana aliirejesha faili iliowasilishwa katika afisi yake.