Mpeperushaji bendera wa Chama cha Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga ameelezea imani yake kwamba ataibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9, mwaka huu.
Akihutubu baada ya kupokea maazimio ya Miungano ya Vyama vya Wafanyakazi chini ya COTU, Odinga ameahidi kutekeleza ahadi zote anazotoa kwa Wakenya.
Ameahidi kuboresha mazingira ya kufanyia kazi nchini, akiongeza kwamba ataimarisha teknolojia kufaulisha utoaji wa habari za kihalifu moja kwa moja kupitia mitandaoni badala ya kuripoti katika vituo vya polisi.
Kwa upande wao viongozi wa miungano hiyo wakiongozwa na Francis Atwoli sasa wameapa kuendesha kampeni kote nchini kupigia debe azma ya Odinga kuwa Rais kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Wakati wa mkutano ulioitishwa na Atwoli, miungano hiyo imewasilisha maazimio yao kwa Odinga, wakitaka yashughulikiwa punde atakapotwaa urais.
READ MORE
Game of chess as titans scramble for Nyanza and Western
Battle for Baba's party heats up as rival ODM faction lands in Kisumu
ODM plans youth convention to chart way forward amid rift with UDA
Six months in death: How politicians are fighting for own survival in post-Raila era
Atwoli amesisitiza kuwa Odinga ndiye atakayekuwa Rais wa tano, akipuuza Muungano wa Kenya Kwanza.