Mbunge Maalum Gideon Keter ameapa kumchukulia hatua za kisheria Mshirikishi wa Serikali eneo la Bonde la Ufa George Natembeya kwa madai ya kuwadhulumu wakazi wa Msitu wa Mau.

Keter amemlaumu Natembeya kwa kuzitesa familia 1, 200 ambazo zimepata hifadhi kutoka kwa msamaria mwema kwenye eneo la Kuresoi baada ya kufurushwa kutoka msitu huo. Akizungumza alipozitembelea familia hizo, Keter amesema amemwangiza wakili wake kuanzisha shughuli ya kumshtakiwa Natembeya.

Keter amesema wakili huyo atawapa wa viomgozi wa serikali katika Msitu wa Mau agizo la mahakama kusitisha shughuli hiyo . Mbunge huyo amesema  wakazi wanaoishi katika msitu huo na Wakenya wanaostahili kulindwa kwa mujibu wa serikali.


Haya yanajiri huku Natambeya, akisema watahiniwa wa mtihani wa darasa na nane KCPE katika Msitu wa Mau hawatafanya mtihani huo hapo kesho.


Amesema kinyume na taarifa kuwa watahiniwa kutoka shule kumi na tano katika msitu huo watafanya mtihani kuanzia kesho, hakuna atakayeufanya, kwani shule hizo zilijengwa pasi na kuzingatia sheria na kwamba si mali ya serikali.