Kwa wale ambao ni wapenzi wa filamu za wasanii wa Nigeria bila shaka wamezowea kuona mila na utamaduni wa watu wa Nigeria zikiigizwa kwa mapana na marefu.
Kuna kiongozi wa ukoo Fulani ama mfalme ambaye huko kwao anajulikana kama Igwee na yeye ndiye anayefanya maamuzi yote na kutekeleza sheria kwa mujibu wa mila zao na huwa ndiye anayesikizwa na wote huku akiwa na serikali yake na baraza lake la mawaziri.
Kisha kuna Kuhani mkuu ambaye anasimamia masuala yote ya kiitikadi na matambiko yote yanayopasa kufanywa na huwa ana madhabahu yake. Sasa mfumo kama huo ulikuweko katika Jamii ya Mgiriama katika wamijikenda na mpaka sasa ungaliko kwa wale ambao ni wana utamaduni katika jamii hiyo.
Kwa kutoa mfano utakaoeleweka kwa urahisi zaidi kwanza na hao watizamaji filamu za kutoka Nigeria, huyo Igwee wao kwa Mgiriama alikuwepo na anajulikana kama Vaya na huyo Kuhani wake mkuu anajulikana kama Gohu.
Kama hao wa huko Nigeria, wanatekeleza mila zao ipasavyo na huwa wana mavazi yao rasmi ambayo watu wengi kutoka jamii hiyo ya wamijikenda hawayajui mavazi hayo wala hawawatambui tena kutokana na muingiliano wa mila za
READ MORE
Chinese EV makers target Nigeria as Africa manufacturing race intensifies
Morocco beat Nigeria on penalties to reach Africa Cup of Nations final
Iwobi hails Nigerian 'unity' with Super Eagles set for Morocco AFCON semi
CAF opens disciplinary investigations into AFCON 2025 quarter-finals misconduct
kigeni zilizosambaratisha sanaa hizo na turathi na utamaduni.
Wagiriama walikuwa wakiamini na mpaka sasa wale wadumishaji wa mila yao wanaamini kwamba kuna maisha baada ya mtu kufariki.
Roho yake inakwenda kukaa mahali na hapo inafanana na ile imani ya kidini kwamba kutakuwa na siku ya Hukumu ambapo roho zote zitakuwepo tena.
Kwa huyo Mgiriama kuna mila moja ya zamani ambayo mpaka sasa inafuatwa ambapo wale waliokufa wanaishi kwa mfumo wa sanamu zilizo na nakshi maalumu ambazo huchongwa na wana itikadi walioteuliwa kufanya kazi hiyo kupitia tambiko maalumu.
Miti huchaguliwa huko msituni na wazee walio na ujuzi huo na inapofikishwa nyumbani huwa si miti tena bali ni viumbe hai wanaotangamana na wale walio hai na huwekwa katika kibanda maalumu katika mji.
Watalii kutoka Marekani na Uingereza walizichukua baadhi ya sanamu hizo kutoka nchi ya Wagiriama mnamo 1985 na kwenda nazo kwao baada ya sanamu hizo kuibwa na vijana wahuni walio wauzia sanamuhizo. Watalii hao walikuwa wamevutiwa na nakshi za vigango hivyo na koma.
Baada ya miaka kadhaa sanamu hizo ziliwahangaisha sana waliokuwa nazo na ililazimu zirejeshwe katika sehemu ya Chalani Kaloleni Giriama.
Kwa mujibu wa Mwarandu bado kuna zengine ambazo zitarejeshwa hivi karibuni kwani wazee hao bado wanawasumbua wazungu huko Ulaya wakitaka kurejeshwa nyumbani na kufanyiwa tambiko la kuwatuliza.
Nilisimuliwa hayo yote na Katibu Mkuu wa Chama cha utamaduni cha Malindi MADIKA Joseph Mwarandu ambaye ni mwana itikadi wa jamii ya Kigiriama.
Sanamu hizo kama alivyonieleza Mwarandu zina majina yake maalumu. Kama mtu alikuwa Kuhani Mkuu yaani Gohu basi huchongewa sanamu inayojulikana kama Kigango kwa kigiriama na kama alikuwa mkuu wa Jamii yaani Vaya ama mzee mwenye cheo Fulani cha jamii hiyo basi huhongewa sanamu inayojulikana kama Koma.
Wanapofanya maombi yaani Ulombi basi wagiriama huanza kwa kuwaombea hao waliotangulia ndipo wakafanya maombi yao. Miti hiyo ambayo nimeiita sanamu ili ieleweke haraka kwao si sanamu bali ni viumbe vilivyo hai katrika vibanda vyao vinavyojulikana kamaVigojo.
Kwa Mgiriama miongoni mwa viumbe walio hai ni hao watu ambao hawajafariki na “sanamu” hizo na pia vijusi.
Kwa mgiriama mwanamke mja mzito haruhusiwi kutoa mimba kwa mujibu wa mila kwani kiumbe aliye naye tumboni ni kiumbe hai.
Baada ya hao wazee kuaga dunia, ni jukumu la washiriki wa familia kwenda kufanya tambiko maalumu la kutengeza sanamu hizo na kuwarejesha nyumbani. Wasipofanya hivyo basi wazee huwatokea ndotoni na kuwasumbua hususan kama walikuwa Gohu ama Vaya na hukumbwa na masaibu chungu nzima.