Uzinduzi wa kampeni ya kusajili kupata vitambulisho maarufu kama #TokelezeaID mjini Kisumu na Katibu Mkuu wa ODM Ababu Namwamba, ni mojawapo ya mikakati itakayohakikisha kuwa muungano wa CORD unatwaa ubingwa katika kiti cha urais ifikapo 2017.
Hata hivyo utafiti na shirika la Ipsos Synovate umeonyesha kuwa ngome tatu kuu za muungano wa CORD zinavuta mkia katika usajili wa wapiga kura unaoendelea. Uzinduzi wenyewe umefanyika wakati amabapo vigogo wa muungano huo wameanza kuhakikisha wafuasi wao wamesajiliwa kupiga kura ili kushindana na wapinzani wao katika muungano wa Jubilee.
Licha ya wito unaotolewa na vinara wa CORD kwenye mikutano ya hadhara, wafuasi wao wamekuwa wakisusia kujisajili kama wapiga kura pasi na kujua umuhimu wake. Pengine hatua aliyoichukuwa Katibu Mkuu wa ODM Ababu Namwamba hivi majuzi itahakikisha kuwa ngome za CORD zinasajili wapiga kura wengi.
Hivi majuzi tumeshuhudia chama cha ODM kikifanya mikutano ya faragha na baadhi ya viongozi wa eneo la Kisii ili kusaidia kuupiku muungano wa Jubilee. Ni bayana kuwa ODM i mbioni kuweka kapuni kura zote za eneo la magharibi mwa Kenya. Swali kuu likiwa ni je, uzinduzi wa kampeni ya #TokelezeaID inaupa nafasi kubwa muungano wa CORD kutwaa kura nyingi ifikapo 2017?
READ MORE
Tubi Vs Bina: UDA's Tubi Jnr wins Isiolo South MP seat after heated family contest
From Stephen Lelei to Katitu and Patrick Shaw: The rise and fall of famed 'super' cops
UDA dismisses United opposition as 'agenda-less' after by-election victories
KMPDC employee arrested as SHA fraud investigations intensify