Bei ya gesi inatarajiwa kuongezeka kwa hadi shilingi 400 mwezi huu.

Tayari Kampuni ya Mafuta ya Rubis imetangaza bei mpya ambayo imeongezeka  kwa shilingi 400 kulinganisha na awali.

Kwa mfano, kujaza mtungi wa gesi wa kilo 6 uliogharimu shilingi takribani 1, 200 sasa utagharimu shilingi 1, 500.

Mtungi wa kilo 13 katika vituo vya Rubis utauzwa kwa shilingi 3, 340.

Hali hiyo inatarajiwa kushuhudiwa katika kampuni nyingine kadhaa za kuuza gesi huku ongezeko la bei ya gesi na bidhaa za mafuta likishuhudiwa kote duniani.

Hata hivyo, ongezeko la bei hiyo nchini limeachangiwa zaidi na kodi ya ziada VAT inayotozwa bidhaa za mafuta.