Kwa miaka kadhaa sasa, kituo ukipendacho cha Radio Maisha kimezidi kutamba, kutaratamba na kutawala tasnia ya utangazaji. Sawa na mwaka jana, mamilioni ya Wakenya wamepiga kura kupitia shughuli iliyosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano, CA na kuichagua Radio Maisha kuwa namba moja kote nchini, chaguo la wananchi.
Kilichofuata ni vigelegele, tabasamu,mwendo wa jiwa na minenguo ya viuno kutoka kwa kikosi cha Radio Maisha kikiongozwa na Mkuu wa kituo hiki, Tom Jappani hadi jukwaani kupokea kombe la ushindi. Aidha Radio Maisha ilituzwa kuwa nambari mbili nchini kwa habari za kuaminika.
Kwa niaba ya usimamizi wa Radio Maisha ikiongonzwa na Tom Japani, Msimamizi wa Vipindi, Linda Oriaso, Mhariri Geofrey Mungou na shirika zima la Habari la Standard Group, PLC, tunachukua fursa hii kusema ahsante kutoka kilindi cha nyoyo zetu kwako wewe uliyesema kwa sauti kuu kwamba kwa hakika, Radio Maisha ndilo chaguo la wengi, chaguo la mwananchi. Tunakuahidi mtangazo bora hata zaidi kwenda mbele. Tunakulaji na kukuthamini ewe msikilizaji. Radio Maisha, Radio zaidi ya Radio, Tuko Mbele Pamoja.