Mkurugenzi wa Kenya Pipeline kuondoka
By Mate Tongola
| Dec. 4, 2018
Nairobi, Kenya,
?
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kenya Pipeline, Joe Sang amesema atajiuzulu baada ya muhula wake wa kuhudumu kukamilika mwezi Aprili mwaka ujao.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, John Ngumi amesema amepokea na kukubali waraka wa Sang ambaye amefafanua kuwa kutokana na sababu za binafsi, hatawania muhula wa pili katika wadhifa huo.
Taarifa hiyo imejiri wakati uchunguzi unaendelezwa kubaini hasara ya shilingi zaidi ya milioni tano kati ya mwaka huu na uliopita.