Na Mate Tongola   Maafisa wa Idara ya Uplelezi, DIC kwa sasa wanaendelea kumhoji Gavana wa Migori, Okoth Obado kufuatia kisa cha kuuliwa kwa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo, Sharon Otieno.   Hii ni mara ya pili kuhojiwa kwa Gavana huyo ambaye ametajwa pakubwa na mauaji hayo. Kuhojiwa kwake leo hii kunajiri baada ya uchunguzi wa VINASABA yaani DNA kubainisha kuwa ujauzito wa marehemu Sharon ulikuwa wake.   Ikumbukwe msaidizi wa Gavana Obado, Michael  Oyamo na aliyekuwa Mwakilishi Wadi wa Kanyadoto, Lawrence Mula ni miongoni mwa washukiwa wa mauaji hayo ambao wanaendelea kuzuiliwa.