Edith Vethi Nyenze, mjane wa aliyekuwa Mbunge wa Kitui Magharibi marehemu Francis Nyenze ndiye mrithi wa kiti hicho.
Edith wa chama Wiper ametangazwa mshindi wa uchaguzi mdogo uliofanyika jana kwa kupata kura 14,372 huku akiwashinda wagombeaji wengine wanne kwa wingi wa kura.
Akitoa tangazo hilo James Mbai, msiamazi wa uchaguzi katika neneo bunge hilo amesema Edith alifuatwa na Dennis Mulwa mgombea huru kwa kura 2,046, Mutiso Lelli wa Narc-Kenya akawa wa tatu na kura 1,784. Wengine ni Fridah Mutui KSC kura 1,075 na wa mwisho akawa Elijah Kilonzi wa CCU na kura 499.
Hata hivyo, idadi ya wapiga kura waliojitokeza kushiriki shughuli hiyo ilikuwa 19,776 ikiwa ni asilimia 38. Eneo bunge hilo lina wapiga 52,042 na vituo vya kupigia kura 143.
Kwa upande wake mbunge mteule Edith ameapa kufanyakazi pamoja na washindani wake kwa manufaa ya wakazi wa eneo hilo huku akishukuru uongozi wa chama cha Wiper kwakumpa nafasi ya kurithi kiti alichokiwacha mumewe