Mwaniaji wa urais wa Chama cha Azimio la Umoja One Kenya ,Raila Odinga amekatiza ghafla ziara yake nchini Marekani ili kurejea Kenya Jumatano wiki hii kuhudhuria mazishi ya Hayati Mwai Kibaki.

Odinga na ujumbe wake akiwamo Martha Karua, Wyliffe Oparanya, Gavana wa Kisii James Ongwae, Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang na Mbunge wa Kathiani Robert Mbui waliwasili Jijini Washington DC Jumamosi ambapo walifaa kuwa nchini humo kwa kipindi cha wiki moja.   Katika vikao vyake vya kwanza, Odinga alikutana na mshauri wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mauaji ya kimbari Anne Wairimu.   Pia alikutana na aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Kenya, Michael Ranneberger baada ya kufanya kikao cha makaribisho na baadhi ya Wakenya wanaoishi Marekani ambao wameeleza matarajio yao kwa uongozi wa Raila iwapo atatwaa urais Agosti 9 2022.