By Standard Digital
| Jul. 10, 2010
Ni miaka kumi na sita sasa tangu nchi ya
Rwanda kukabiliwa na vita vya kikabila kati ya makabila makuu ya wahutu na watutsi. Na japo bado wangali wana safari ndefu kabla ya kuwa na uwiano kikamilifu kati ya wanyarwanda,nchi hii imepiga hatua za kusifika. na japo Rais Paul Kagame amekuwa akishutumiwa kwa kuzuia demokrasia na kuwanyima wanahabari Uhuru wa kujieleza,Kagame anajitetea kuwa yote haya anafanya kwa minajili ya kuzuia vita vingine vyovyote nchini humo. Mwanahabari wetu Carol Nderi alikuwa nchini Rwanda
na ametuandalia taarifa ifuatayo.