Kwa mara ya kwanza kabisa, Serikali ya Tanzania imeashiria kuwa Rais John Pombe Magufuli anaugua.
Licha ya awali viongozi wakuu kukana taarifa kwamba Magufuli amelazwa kutokana na Ugonjwa wa Covid, Makamu wa Rais waTanzania mama Samia Hassan Suhulu amesema kwamba ni kawaida kwa binadamu yeyote kugua maradhi kama vile homa na mafua.
Akizungumza wakati wa mkutano wa umma, Samia hata hivyo, amesema kwamba Tanzania i salama na kuwataka wananchi kutokuwa na hofu.
Wakati uo huo, amewataka kushikamana na kupuuza taarifa za mataifa mengine kuhusu afya ya Magufuli. Amesisitiza haja ya Watanzania kukumbatia shughuli za ujenzi wa taifa na kupuuza propaganda.
Magufuli mwenye umri wa miaka sitini na mmoja na ambaye amekuwa akitilia shaka uwapo wa janga la Korona, hajaonekana hadharani kuanzia Februari 27 mwaka huu huku tetesi zikiibuka kwamba amelazwa akiigua Covid-19.
READ MORE
The trouble with Tanzanian president's 'mikwaju' proposal
Djibouti raises stakes with Sh20.7b Fuelstor energy hub
Kenya moves to strip trade barriers at Migori border crossing
Pipeline politics: Why East Africa's joint refinery dream faces slippery path
Watanzania kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakiendeleza shutma dhidi ya Kiongozi wa Upinzani Tundu Lissu kufuatia madai yake kwamba Magufuli amelemewa na ugonjwa wa Covid-19 na aamesafirishwa kuelekea India kwa matibabu zaidi.
Mapema Mei mwaka uliopita Magufuli alitangaza kwamba taifa lake limefanikiwa kudhibiti korona kupitia maombi licha ya taarifa kuwapo kuhusu idadi kubwa ya watu wanaofiriki .
Aidha, alisitisha shughuli za kutoa takwimu za maambukizi ya kila siku jinsi yanavyofanya mataufa mengine Afrika na Dunia.