Mbunge wa Nakuru Mjini Mashariki Samuel Arama amekamatwa. Mbunge huyo anaendelea kuzuiliwa katika kituo cha Polisi cha Railways ambapo anaendelea kuhojiwa na maafisa wa Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi EACC kwa ushirikiano na maafisa wa polisi. Kulingana na nduguye Charles Arama ambaye yuko kituoni humo Arama alitiwa mbaroni na maafisa wa EACC jana usiku alipokuwa katika klabu moja mjini NAakuru.
Inaarifiwa mbunge huyo pamoja na wakili wake Kennedy Onkoba walikamatwa kwa kukiuza kipande cha ardhi kinachomilikiwa na kampuni ya Eveready.
Wafuasi wa Mbunge huyo pamoja na jamaa zake wako nje ya kituo hicho wakitaka aachiliwe. EACC imesema wanawatafuta washukiwa wengine waliohusika katika sakata ya uuzaji wa kipande hicho cha ardhi.