Vita kati ya Beka na Aslay wa Yamoto Band
Duh! Bongo kimenuka sasa yaani ni vita kati ya wasanii wa Yamoto band punde tu baada ya kusambaratika.
Bendi hio iliyojumuisha wasanii wanne wenye uwezo mkubwa kwenye game la muziki sasa wameingia bifu za huku kiongozi wao Aslay akionekana kuwafunika wenzake.
Aslay mkali huyo wa Yamoto amekuwa akiachia ngoma mfululizo bila kuwapa nafasi wenzake na sasa mmoja wao,Beka ametangaza vita na Aslay.
Beka Flavour mwimbaji wa 'Libebe' amefunguka kupitia kituo kimoja cha runinga Tanzania na kusema kuwa alikuwa amepanga kuachia ngoma yake mpya juzi wakati Aslay alimtangulia na ngoma yake 'Baby'. Beka amewaka wazi kuwa wiki mbili zijazo ataachia dude lake hata kama Aslay akitoa nyingine, bora zikutane.
READ MORE
Kenya's future depends on citizens daring to act with hope and virtue
Why the noises of the Kenyan choir needs a master to harmonize it in 2026
Let's not bury Jirongo until questions around his death have been answered
“Nikimwambia atulie mimi kama nani kwenye uongozi wake, kwa hiyo ni kitu ambacho amepanga yeye na uongozi wake kutoa bam to bam kwa hiyo mimi naona sawa, aendelee kutoa tu. Akitoa baada ya wiki mbili mbele hapo siwezi kusubiri na mimi natoa mashine,” amefunguka Beka.
Hata hivyo amekiri kuwa sio kwamba anamwogopa Aslay kama watu wanaofikiria na wala muziki wake ulengi msanii huyo.
“Kwa sababu mimi ndio nimepanga wiki mbili mbele kwa hiyo akitoa tena siyo mbaya zikipambana. Hamna wale wanye fikra kuwa nimemuogopa waendelee kufikiri hivyo, halafu muziki wangu sija-focus kwa yeye na-focus kwa watu wakubwa wengine wa nje,” amesisitiza.
-Na,MkazivaeUNIT