Na Stephen Mukangai.
Wenyeji wa fainali za kombe taifa bingwa barani Afrika, Makala ya 31, Gabon wameyaaga mashindano hayo.
Gabon imeyaaga mashindano hayo baada ya kuambulia suluhu dhidi ya Cameroon kwenye mechi ya mwisho ya kundi A. licha ya kuonesha mchezo mzuri Gabon walishindwa kuzitumia vizuri nafasi zao na hivyo kuwapa Cameroon tiketi ya moja kwa moja.
Gabon ni timu ya pili kuyaaga mashindano hayo baada ya Uganda Cranes.
Kwenye matokeo mengine Burkina Faso iliikung’uta Guinea Bissau magoli mawili kwa nunge. Wachezaji Silva na Traore walipachika wavuni goli moja kila mmoja.
READ MORE
Gabon fashion designer brings traditional raffia to Paris runways
Facebook, TikTok inaccessible as Gabon shuts down social media
Gabon government suspends entire national team after winless AFCON exit, Aubameyang dismissed
Defending champions Ivory Coast overcome early shock to finish top of AFCON Group F
Kufuatia matokeo hayo timu za Cameroon na Burkina Faso zimefuzu kwenye hatua ya robo fainali.
Jumatatu mechi za kundi B zitaingia awamu ya tatu hatua ya muondoano ambapo katika mechi ya kukata na shoka Senegal itakabana koo na Algeria kisha Tunisia imalize udhia na vijana wa Robert Mugabe kwa maana ya Zimbabwe.