Wakenya wametakiwa kujiunga na mataifa mengine katika utunzaji wa mazingira ili kukabili athari za mabadiliko ya hali ya anga.

Akizindua kongamano la kujadili mabadiliko ya hali ya anga Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago amesema kuwa ni wajibu wa kila Mkenya kuhakikish kuwa mazingira yanatunzwa.

Mandago amewataka viongozi wa humu nchini kuwaelimisha Wakenya kuhusiana na utunzaji wa mazingira.

Kauli yake imesisitizwa na Afisa Mkuu Katika Wizara ya Maji Na Mazingira katika Kaunti ya Makueni Mary Mbenge ambaye ametoa wito wa kuwekwa mikakati ya haraka ili kuhakikisha kuwa mazingira hayaharibiki.