Kaunti ya Nairobi inataka maagizo ya mahakama kuwaruhusu kuwarejesha nchini mwao omba-omba waliokamatwa katikati ya jiji la Nairobi wakati wa oparesheni iliyoendeshwa kulisafisha jiji hili.

Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Masuala ya Elimu, Jinsia na Vijana kaunti hii Janet Ouko, omba-omba wengi waliletwa nchini kinyume na sheria kutoka mataifa ya Tanzania na Uganda.

Tayari watu saba walikamatwa mtaani Huruma jana kwa kuwatumia omba-omba hao kuwalaghai wakazi, na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kuendesha shughuli zilizopigwa marufuku.