Ni rasmi sasa koti tamba ya Emuhaya/Luanda imezinduliwa ili kwa kutoa huduma kwa wakazi wa eneo hilo kuanzia wiki ijayo pasi na kusafiri mwendo mrefu kufika mahakama ya Vihiga na Maseno mtawalia na la mno kuashiria kupunguza idadi za kesi zinazorundika kwenye koti hizo pasi na kushughulikiwa.
Akizindua koti hiyo tamba eneo la Mulukhoro eneo bunge la Luanda, hakimu mkuu wa mahakama ya Kakameka na Vihiga kwa mpigo Bi. Ruth Sitati amedokeza kuwa nia na lengo haswa ya kufanya hivyo imetokana na kufurika kwa kesi ambazo hutoka katika kituo cha polisi cha Luanda na pia mwendo wa kusafiri maeneo ya koti za maseno na Vihiga umekuwa na ati ati swala linalosababisha utendakazi kuwa na utatanishi.
READ MORE
KNBS to do first census on TVET institutions in 63 years
800 youth benefit from 'Glam on Wheels' Initiative
Togo scraps 30-day visa requirements for African countries
Relief for commuters as matatu strike suspended for one week
Aidha, amedokeza kuwa kupitia kamati teule ya haki kila mteja ama au mkenya yeyote yule ana haki ya kupata haki ya kuhudumiwa karibu na maeneo yao, ambapo wanazidi kuzindua koti hizo tamba maeneo mengine katika mkoa wa magharibi mwa kenya.