Ikiwa njia mojawapo ya kukabili changamoto zizazowakumba wawekezaji kutoka mataifa ya kigeni humu nchini , Serikali inalenga kuboresha mazingira ya kibiashara ili kuwavutia wawekezaji wataobuni nafasi za ajira kwa vijana.

Ndiyo kauli ya Waziri wa Viwanda na Biashara Peter Munya.

Akizungumza katika eneo la Viwanda ya vya kutengenezea bidhaa za kuuza nje ya nchi EPZ-A katika eneo la Athiriver kaunti ya Machakos, Waziri Munya amesema serikali imepunguza gharama za umeme kwa wawekezaji kwa asilimia thelathini, pamoja na kuunda miundo msingi bora ili kuboresha sekta ya uzalishaji nchini.

Wakati uo huo Mwenyekiti wa Bodi ya Halmashauri ya EPZ- A Paul Gicheru, amesema serikali matatizo ya uhaba wa maji na mkondo wa taka kwa yameshughulikiwa kwa kuboresha usambazaji maji kwenye viwanda vyote nchini.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mkuu wa Ujerumani Tarek Al Wazir, amesema taifa lake litawapa vijana kipao mbele wakati wa kuwaajiri wafanyakazi katika kiwanda kilichozinduliwa ili kutengeneza bidhaa za kuuzwa nje ya nchi hii.