Mengitis ni uvimbe wa sehemu iitwayo mengines katika ubongo na uti wa mgongo. Uvimbe huo husababaisha kuumwa na kichwa, joto jingi mwilini na kuumwa na shingo, na usipogunduliwa mapema huisababisha kifo.
Menengitis husababishwa na bakteria, maambukizi ya virusi, na maambukizi ya vimelea yaani fungal infection. Vilevile kando na ubongo na uti wa mgongo maambukizi ya menengitis vilevile hutokea katika sehemu mbali mbali mwilini kama masikio, koo na sinuses.
Menengitis ya Bakteria ndio hatari zaidi kwani isipotibiwa kwa haraka husababisha kifo na matatizo ya ubongo, vilevile huathiri yeyote aliye karibu na anayeugua , sana sana wanafunzi au askari walio katika mabweni. Kwani husambazwa anayeugua anapokohoa au kupiga chafya.Bakteria anayesababisha menengitis husasambaa katika damu hadi kwa ubongo kutoka kwa masikio, koo au sinuses.
Aina ya pili ya maambukizi ya virusi yaani viral menengitis. haina makali sana ikilinganishwa na ya bakteria. Mara nyingi huchochewa na virusi kama HIV, herpes, virusi vya west Nile miongoni mwa vingine.
Aina ya tatu ni ya vimelea yaani Fungal Mengitis. Ambayo ni nadra sana kutokea na mara nyingi huathiri walio na matatizo ya kinga mwili mfano UKIMWI.
Mtu yeyote anaweza kupata menegitis hata hivyo walio katika athari zaidi ni watoto waliochini ya miaka mitano, vijana kati ya mika 16-25,watuwazima waliopita mika 55 na walio na maradhi ya muda, upungufu wa kinga mwilini na waliotolewa sehemu ya utumbo iitwayo spleen,ambayo huchuja damu kabla ya kusambazwa mwilini, hivyo kuzuia maambukizi,na wanawake wajawzito.
Dakta Ng'adi Victor Ng'adi anaeleza kuwa dalili za meningitis kwa watoto ni kuumwa na kichwa, kupoteza uwezo wa kusikia,kusahau mara kwa mara, matatizo ya ubongo na figo, kujifunza mambo polepole, matatizo ya kutembea, kilia mara kwa mara, kushindwa kulala na uvimbe katika utosi. Dalilizingine hasa kwa watuwazima ni Kuumwa na kichwa, joto jingi mwilini na kutapika
Mtu anaweza kujikinga na Mengitis, kwa kuosha mkono baada ya kuwa msalani, usitumie na yeyeote vitu kama vinywaji, mirija, lipstick au lipbalm, mswaki na vyombo kama vijiko na umma. Vilevile Ukikhoa au ukipiga chafya funika mdomo na pua.