Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko, hatakuwa debeni katika kinyang'anyiro cha ugavana wa Mombasa.

Uamuzi huo umefanywa na Tume ya Uchaguzi, IEBC ambayo imebatilisha cheti ya kumwidhinishwa Sonko kwa misingi kwamba hafai kushikilia wadhifa wowote wa uongozi baada ya kubanduliwa mamlakani kufuatia utovu wa maadili.

Afisa wa IEBC tawi la Mombasa Yusuf Swalha ambaye awali alimwidhisha Sonko, amesema hatua hiyo inaendana na uamuzi wa Mahakama ya Juu kudumisha kubanduliwa kwake na Bunge la Kaunti ya Nairobi mwaka wa 2022 kutokana na utovu wa maadilili

Kwa mujibu wa Yusufu, Sonko hana uwezo wa kuwania uongozi katika Kaunti yoyote nchini baada ya cheti cha uteuzi wake kubatilishwa.

Sonko alikuwa ameidhinishwa na Yusuf kuwania ugavana wa Moambasa, kufutia agizo la Mahakama Kuu ya Mombasa iliyosema alifungiwa nje ya kinyang'anyiro kinyume na sheria licha ya kutimiza mahitaji yote ya kuwania.

Tayari Sonko amewasilisha kesi katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki akipinga uamuzi wa Mahakama ya Juu kwa misingi kwamba ulikiuka haki zake.