Kumekuwa na mabadiliko mob sana ukilinganish na mambo za kale.
Lakini kuna zile mila ama mambo bado watu fulani wamezidi kushikilia kama glue. Unapata mtu bado ameshikila mila na yet imeptwa na wakati.
Kwa mfano, kitambo ungenyorosha mtoto wa wenyewe ukimpata akifanya makosa. Jaribu leo kuguza mtoto wa wenyewe ndio utajua kwa nini punda hushonde sausages na imekula nyasi. Vitu zimebadilika.
But leo unapata kuna watu bado wameshikilia hizo vitu za kale mpaka waleo. Kuna zile mila ama tabia zinaturudisha sisi wakenya nyuma. Mimi sisemi eti mtu asifuate mila na desturi za kwao juu tulishaambiwa eti muacha mila ni mtumwa.
Kitu najaribu kusema ni eti isikuingie sana kwa damu — too much of something is dangerous.
Kuna watu wengine wanafuata hizo vitu za kitambo lakini wanafuta kimaembe maembe. Eti uko na gari lakini hauwezi ukaenda nayo ocha kwenu eti utarogwa. Ukienda nayo unaiwacha town ndio uingie mushatha na nduthi ama kiurastaman troading.
Kwa nini mtu akuroge kwa sababu ya mali yako? Watu kama hao mnafaa mjue maendeleo haiwezi ikapatikana kama bado mko na hio mtaa mentality ya kurogana.
Wengine wameshikilia mila kiumwehu ni hawa watu wameoa. Unapata jama ameoa but ameshikilia eti hawezi akalala kwa akina bibi, eti afadhali atoke usiku wa manane, hata kama ataibiwa yeye hajali.
Eti hawezi kudoze kwa akina woman wake juu mila hairuhusu. Kama wewe ni mtu kama huyu lazima ujue hizo enzi ziliisha na unaweza ukalala kwa akina bibi.
In fact, hata dowry siku hizi watu hawaitishwi. Na kama imeitishwa, inalipiwa hata kwa bar. Zamani dowry ilikua ni kama biashara. Ukipeleka dowry uko na wasiwasi juu utakuta wanyanye wamekungojea na bills noma. Ma uncles za bibi pia wanadai. Then baba ya bibi anamalizia kwa kuitisha dowry. Unaitishwa mamillioni hapo mpaka unashindwa kama umeoa mabibi saba ama ni mmoja tu. Lakini siku hizi ni free style, ukipata dowry peleka ukikosa hustle mapaka siku ile utaiwahi upeleke.