KCSE 2011 begins
By Standard Digital
| Oct. 19, 2011
Mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne mwaka huu ilianza rasmi saa mbili na nusu asubuhi ya leo. Hata hivyo hali haikuwa shwari kwa wanafunzi 40 wa shule moja ya kibinafsi mjini kisii kisii baada ya kuhadaiwa na uongozi wa shule hiyo ambao haukuwasajili wanafunzi hao kwa mitihani hiyo. Shule hiyo kwa jina upbridge academy ilikosa kuwasajili wanafunzi hao bila kuwataarifu, kwa kisingizio kwamba baadhi yao walikuwa wazembe darasani na kwamba wangefeli hata ikiwa wangefanya mitihani hiyo.