Kinyanganyiro cha eneo bunge la Kirinyaga ya kati kilionekana kuwa
kama uzinduzi wa siasa za mwaka 2012 kwenye eneo la kati huku ushindi wa chama cha PNU ukionekana kuwa pigo kwa mbunge wa Gichugu Martha Karua. Katika uchaguzi huo Joseph Gitari aliibuka mshindi baada ya kumshinda mgombeaji wa chama cha NARC Kenya Daniel Karaba kufuatia uchaguzi uliodaiwa kukumbwa na madai ya utoaji hongo kutoka pande zote mbili.