Meya wa baraza la jiji la Nairobi Geoffrey Majiwa aliyetiwa mbaroni na maafisa wa tume ya kupambana na ufisadi nchini mapema leo kwa tuhuma za kuhusika katika kashfa ya ufisadi atalazimika kulala seli hadi kesho anapotarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.Tayari majiwa ameandikisha taarifa kuhusiana na kashfa hiyo ya ununuzi wa ardhi iliyotarajiwa kutumika kwa makaburi ya umma. Zubeidah Kananu amekuwa mbioni siku nzima kufuatilia taarifa hiyo na sasa anatupa uhondo kamili.
Kashfa Ya Maziara
By Standard Digital
| Oct. 26, 2010