Yaliyomo michezoni: Lewa Marathon; 03/07/2011
By Standard Digital
| Jul. 4, 2011
Kila mwaka maelfu ya watu kutoka kote barani Afrika hupiga kambi katika mbuga ya wanyama ya Lewa kwa lengo la kushiriki mbio za Safaricom Lewa Marathon. Na kando na fedha zinazowaendea washindi, lengo kuu la mbio hizi ni kuchangisha fedha za kuhifadhi mbuga hiyo. Na baada ya makala ya mwaka huu kufanyika jumamosi iliyopita leo hii tunaangazia matunda ya mbio hizo tangu zilipoanzishwa.