Kinara wa Chama cha CCM, Isaac Rutto amesisitiza kwamba anamuunga mkono Naibu wa Rais, William Ruto kutokana na sera zake wala si kwa sababu anatoka Jamii ya Kalenjin.

Akihutubu katika Kaunti ya Bomet, Ruto aidha ameendelea kushtumu kauli ya Rais Uhuru Kenyatta kwamba nafasi ya uraisi inapaswa kuwachia makabila mengine nchini.

Wakati uo huo, ameitaka serikali kushughulikia maslahi ya wahudumu wa afya wanaogoma ili kuwasitishia wananchi mahangaiko.

Ikumbukwe Ruto ndiye gavana wa kwanza wa Bomet.