Mfanyabiashara raia wa Uholanzi Tob Cohen atazikwa Jumatatu wiki ijayo katika hafla itakayofanywa faraghani katika makaburi ya Wayahudi jijini Nairobi.

Mawakili wa familia ya mke wa marehemu Philip Murgor na Cliff Ombeta wa familia wameafikiana kuhusu hatua hiyo pamoja na kwamba mke wa Cohen Sarah Cohen pamoja na dada ya Cohen Gavrie watahudhuruia mazishi hayo.

Aidha, wameafikiana kwamba mazishi hayo yatafanyika kuendana na tamaduni za wayahudi huku Mkuu wa Mashtaka ya Umma, na Idara ya Upelelezi, DCI wametakiwa kuendesha uchungizi wa kina kuhusu mauaji hayo.

Maafikiano haya yanajiri wakati qanapatholojia walioupasua mwili wa Cohen wakidokeza kwamba tayari wamebaini kilichomuua japo hawataweka wazi kwa umma matokeo hayo kutokana na agizo la mahakama.

Shughuli hiyo iliendeshwa jana kwa zaidi ya saa nne na kuongozwa na Mwanapatholojia Mkuu wa Serikali, Dkt. Johansen Oduor ambaye alisema kwamba tayari wamebaini alivyouliwa.