Na, Sophia Chinyezi
Moussa Faki Mahakama, Waziri wa Masuala ya Nje wa Chad ndiye Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja wa Afrika AUC.
Mahamat ameteuliwa kwa wadhifa huo baada ya kumshinda Waziri wa Masuala ya Nje wa Kenya Amina Mohammed ambaye alipata kura 26 dhidi ya 38 alizopata.
Hayo yakijiri Rais wa Guinea Alpha Conde amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Umoja wa Africa AU. Wadhifa huo ulikuwa ukishikiliwa na Idris Debi wa Chad.