Rais Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika mashirika mbalimbali ya serikali ambapo amemteua aliyekuwa mgombea mwenza wa urais wa Peter Kenneth Ronald Osumba kuwa mwenyekiti mpya wa bodi ya Hazina ya Vijana.
Aliyekuwa Mbunge wa Bumula, Bifoli Wakholi aidha ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Shirika la Kilimo huku Partrick Osero akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii na Fedha. Aliyekuwa Mbunge wa Changamwe Ramadhan Kajembe, ndiye mwenyekiti mpya wa bodi ya Huduma za Feri nchini.
Wakati uo huo, aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Meja Jenerali Julius Karangi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Viwanja vya Ndege Nchini, KAA. Karangi ataanza rasmi majukumu yake Julai ishirini na nne. Wadhifa huo awali ulikuwa ukishikiliwa na aliyekuwa Inspekta Mkuu wa Polisi, David Kimaiyo.
Na Beatrice Maganga
READ MORE
Ruto allies accuse Uhuru of funding Linda Mwananchi
Stop dragging Uhuru's name into political disputes, Gachagua tells Duale
Ruling party UDA accuses Uhuru of plotting to fund mass protests
From watching television to listening to ground; how Uhuru has evolved