Ujenzi kwenye milima ya Lamu watishia vyanzo vya maji
By Standard Digital
| Apr. 22, 2012
Wenyeji wa Lamu wanatoa tahadhari kwa kuendelea kwa ujenzi katika milima ya Shella Lamu ambako ni vyanzo vya maji masafi kwa wenyeji 30,000 wanaoishi kisiwani humo, na kama anavyoripoti Anne Ngugi aliyezuru kisiwani humo hivi maajuzi wasiwasi mkubwa kwa wenyeji ni kuwa mabwenyenye kutoka nje ya nchi na vigogo wakuu serikalini wanaendelea kunyakua ardhi eneo hilo na kutishia matumizi ya maji masafi katika siku zijazo. Sasa wanataka milima ya Lamu kulindwa kupitia gazeti rasmi la serikali ili itambulike sawia na msitu wa mau.