Waziri wa Masuala ya Ndani ya nchi, Fred Matiang'i amelipa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia Wakimbizi, UNHRC makataa ya siku 14 kuwasilisha mpango wa kufungwa kwa kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma.
Aidha, Matiang'i amesema kwamba kamwe serikali haitatoa fursa ya mazungumzo kuhusu agizo hilo ambalo litawaathiri maelfu ya wakimbizi asilimia kubwa ni wa kutoka Somalia wakiwa ni zaidi ya nusu milioni.
Ikumbukwe kuwa si mara ya kwanza kwa serikali ya Kenya kutangaza mpango wa kuzifunga kambi hizo, mwaka 2012 aliyekuwa Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni Amina Mohammed vilevile alitangaza mpango huo ambao ulisitishwa wiki kadhaa baadaye.
Agizo la Matiang'i linajiri siku kadhaa baada ya Kenya kutetea uamuzi wake wa kujiondoa katika kesi inayohusu mzozo wa mpaka wa majini kwenye Bahari Hindi baina yake na taifa jirani la Somalia kwa kutilia shaka uhuru wa mahakama ya ICJ inayosikiliza kesi hiyo.
READ MORE
Barasa calls for mutual respect between governors and senators
Governor Kachapin warn on illegal gold mining in West Pokot
Private security guards fault regulator over pay, working conditions
Floods, conflict disrupt healthcare for chronic disease patients