Wamiliki sitini na saba wa nyumba kwenye kipande cha ardhi Plot Number 106/1/MN kwenye mtaa wa Kongowea Eneo Bunge la Nyali, Kaunti ya Mombasa wanahofia kufurushwa baada ya kupewa notisi ya kuondoka kwenye kipande hicho kabla tarahe mosi mwezi Agosti mwaka huu.
Wamiliki hao wanasema kwamba mnamo tarehe kumi na tano mwezi wa Disemba mwaka 2017, waliwasilisha malalamishi yao kuhusu mzozo huo wa ardhi kwa Idara ya Ardhi na kuahidiwa kwamba suala hilo lingechunguzwa na hatua mwafaka kuchukuliwa ila hadi sasa suala hilo halijafanyika.
Wamiliki hao sasa wanaishinikiza Serikali ya Kitaifa kuingilia kati ili kuhakikisha mzozo huo ambao umedumu kwa muda sasa unatatuliwa kwa njia inayofaa.
Kwa upande wake Clement Wasike msimamizi wa ardhi eneo la Nyali amemshinikiza mbunge wa eneo hilo Mohamed Ali kuingilia kati sual hilo.