Jamii kumi na nane nchini hazijawakilishwa kivyovyote katika ajira zinazotolewa na Tume ya Huduma za Bunge la kitaifa.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya Kamati ya Bunge kuhusu Uwiano na Usawa imedokeza kuwa jumla ya wafanyakazi bungeni ni kutoka jamii 25 pekee. Wabunge Ong'ondo Were wa Kasipul na Jerusha Momanyi wa Nyamira wamekwaza sababu za tume hiyo kukosa kuzingatia usawa wa kimaeneo wakati wa kuwaajiri wafanyakazi wake ikizingatiwa umuhimu wa taasisi hiyo. 

Aidha, Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge maalum Maina Kamanda, imedokeza kuwa jamii ya Kikuyu inaongoza kwa idadi ya wafanyakazi Katika Tume ya Huduma za Bunge, PSC ambapo ni wafanyakazi 164 wakifwatiwa na waluhya ambao ni 126 kisha wa-Luo 90, Kalenjin 82, Kamba 81, Kisii 53, Somali na kadhalika.

Vilevile, imebainika kuwa ni wafanyakazi kumi pekee wenye ulemavu walioajiriwa bungeni.