Mamlaka ya Ubaharia nchini KMA kwa niaba ya Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga Kenya Meteorological imewatahadharisha wavuvi na mabaharia kuwa waangalifu kufuatia mawimbi makali ambayo yalianza kushuhudiwa jana, nayanayotarajiwa kukamilika tarehe 21 mwezi huu.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, mamlaka hiyo imezitaja Bahari Hindi kwenye Kaunti za Lamu, Kilifi, Mombasa na Kwale kuwa zitakazoathirka na hali hiyo. Aidha KMA imewaonya wananchi vilevile kuwa makini ili kuzuia visa vya kuzama baharini.
Onyo hilo linajiri siku tisa baada ya wavuvi wanne kuzama, wakati chombo chao kilipozidiwa na mawimbi makali walipokuwa kwenye shughuli zao za uvuvi kwenye Bahari Hindi ya Nyali Jijini Mombasa. Kufikia sasa wavuvi hao hawajapatikana.