Usiku ni wakati wa raha.Janet Mwaluda wa Nairobi Diaries awajibu Wanaokosoa Kipindi hicho.

Kevin Oduor

Akizungumza katika kipindi cha Konnect Kituo cha Radiomaisha, Janet Mwaluda ambaye ni mwanzilishi wa Kipindi maarufu cha Nairobi Diaries kinachoshirikisha wanamtindo waliobobea nchini,ameitetea show  hiyo na kushikilia kuwa dhamira yake ni kueleza hali halisi katika maisha haswa walio katika uhusiano wa kimapenzi.Ingawa, amekiri kuwa amewai fukuza baadhi ya waigizaji ambao waligura show yake, amesema kuwa angemtaka Prezzo kurujea kwenye game akiongeza kuwa Mwanamuziki huyo alitoka kwa hiari.Licha ya kusomea kozi ya ‘actuarial science ‘ kiwango cha shahada katika chuo kikuu cha JKUAT, Janet amekuwa kielelezo cha wengi akisema kuwa unawezaanzisha mradi wowote na ufauli hata kando na kile ulichokisomea.