Na Suleiman Yeri
Wizara ya Ardhi imezishtumu serikali za Kaunti na Makundi ya kidini kwa kuhujumu juhudi zake za kuzitwaa ardhi za shule, hospitali na misitu zilizonyakuliwa.
Kulingana na Waziri Jacob Kaimenyi serikali nyingi za kaunti hazijafahamu kuwa hati miliki zilizokuwa zimekabidhiwa serikali za wilaya sasa zipo chini ya hazina kuu ya kitaifa.
Aidha waziri ameyashtumu makundi ya kidini kwa kukataa kutoa hatimiliki za shule za umma walizokuwa wakiziongoza na sasa hivi ziko chini ya serikali.
Kaimenyi ameongeza serikali inafanya kila juhudi kuhakikisha inazitwaa ardhi zilionyakuliwa na watu binafsi huku akidokeza kuwa sababu kuu ya ardhi za shule za umma kunyakuliwa ni kwa sababu zipo katika sehemu zenye uvutio mkubwa.
Wakati uo huo amesema kuwa kwa ushirikiano na Tume ya Kitaifa ya Ardhi na Wizara ya Afya wanazikagua ardhi za hospitali zote nchini ili kuhakikisha zinapata hati miliki.