Na Beatrice Maganga

Serikali imezibadili saa za kufunguliwa kwa kontena zinazohifadhi karatasi za Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne KCSE kutoka saa kumi na moja asubuhi hadi saa kumi na mbili unusu asubuhi. Wizara ya Elimu kwa Ushirikiano na Baraza la Kitaifa la Mitihani nchini KNEC wametoa muongozo huo baada ya kubainika kwamba baadhi ya walimu wakuu wamekuwa wakijaribu kufanikisha udanganyifu katika mitihani hiyo kufuatia kukabidhiwa karatasi hizo mapema.
Kwenye taarifa kupitia wa Katibu wa Wizara hiyo Belio Kipsang, walimu na wasimamizi wa mitihani aidha wameonywa dhidi ya kuzungumzia masuala ya mitihani hiyo kwenye mitandao ya kijamii ili kuzuia kuhujumu kufanyika kwa mitihani hiyo kwa njia inayostahili.
Amesema Mwenyekiti wa KNEC George Magoha ndiye pekee aliye na mamlaka ya kuwasilisha taarifa kuihusu mitihani inayoendelea.