Na Beatrice Maganga
Shirika la Ndege la Kenya Airways, limesema abiria waliokuwa wakisafiria mojawapo ya ndege zake iliyokumbwa na matatizo ikiwa angani wako salama. Kwenye taarifa, shirika hilo limesema kwa sasa ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Uganda Jumatatu jioni inakaguliwa na wahandisi. Mojawapo la magurudumu ya ndege hilo lilipasuka ilipokuwa ikitua katika uwanja wa JKIA.
Katika siku za hivi karibuni, misururu ya visa kuhusu hitilafu za ndege imeshuhudiwa nchini. Wiki iliyopita ndege moja ilianguka katika Msitu wa Kibiku Ngong ambapo rubani na mwanafunzi wake walijeruhiwa. Siku chache zilizopita ndege nyingine ya polisi ilianguka katika Mtaa wa Mathare na kuwajeruhi polisi wanne.
Mtalii mmoja aidha alifariki dunia wakati ndege aliyokuwa ameabiri na wenzake kuanguka eneo la Naivasha. Wengine walijeruhiwa wakati wa kisa hicho.