Wambui burial tussle - Swahili
By Standard Digital
| Sep. 2, 2011
Mzozo unatishia kuibuka tena kati ya familia ya s.m otieno na ile ya marehemu wambui otieno kuhusu mahala atakapozikwa wambui. Hii ni kufwatia madai kutoka kwa ukoo wa umira kager ambao unasisitiza kuwa kulingana na mila za jamii ya waluo wambui anapaswa kuzikwa kando ya mumewe huko siaya. Familia ya wambui nayo imesema kuwa wambui atazikwa kulingana na matakwa yake nyumbani mwake huko matasia ambapo wambui alikuwa amejichimbia kaburi miaka ishirini iliyopita. Familia hiyo imetangza siku ya alhamisi kama siku atakayozikwa wambui.